18 Januari 2019 - 17:03
Mmoja kati ya magaidi wakubwa wa Libya auliwa

“Abu-Twalhah” mmoja miongoni mwa viongozi ma magaidi wa Daesh nchini Libya ameangamizwa nchini humo

Shirika la habati AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Libya vimetangaza kuangamia kwa mmoja miongoni mwa viongozi wa kikundi cha kigaidi cha Alqaida nchini Libya ameangamizwa kufutia mpango wa serikali wa kuwaska magaidi hao nchini humo.
Vyanzo vya habari hivyo vimetangaza kuwa “Abdulmunim Salim” aliyepewa lakabu ya “Abu-twalhah” ameangamizwa katika mashambulizi yaliofanywa na majeshi ya Libya, yaliofanyika karibu ya mji wa “Sabahaa” kusini mwa nchi hiyo.
Majeshi ya ulinzi na uslama ya Libya yalishambulia nyumba ya gaidi huyo na kufanikiwa kumsambaratisha yeye na magaidi wenzake waliokuwa wamejificha katika nyumba hiyo.
mwisho/290